24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa dini Simiyu wafanya Ibada kumuombea Magufuli

Na Mwandishi Wetu, Simiyu

Viongozi wa dini Mkoa wa Simiyu wamefanya ibada maalum ya kumuombea Hayati Dk John Magufuli.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Simiyu Emmanuel Silanga akizungumza mkoani Simiyu wakati wa Misa aliyoiandaa maalumu kwa Chama cha CCM mkoani Simiyu kumuombea Hayati Dk John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania jana.PICHA NA MPIGAPICHA WETU

Katika ibada hiyo ambayo ilihudhuriwa na wananchi, watendaji wa serikali na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Emmanuel Gungu.

Akizungumza katika ibada hiyo, Gungu amesema Hayati Rais Magufuli amefanya kazi kubwa hasa katika kuwaletea maendeleo ya Wananchi.

“Hapa Simiyu Hayati Rais Magufuli amefanya Mambo mengi. Ametujengea barabara za lami, miradi mikubwa ya maji Pamoja Na viwanda,”amesema Gungu.

Nae Katibu wa CCM Mkoa Wa Simiyu, Hawra Kachwamba amesema Watanzania wanapaswa kumueni, Dk. Magufuli kwa Mambo mengi mema aliyofanya kwa Watanzania.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mahamud Kalokola alisema Hayati Rais Magufuli alifanya mengi hasa kwa Watu wanyonge ambao kwa kiasi kikubwa alikuwa akiwatetea.

“Hayati Rais Magufuli amefanya Mambo makubwa, alikuwa mtetezi wa wanyonge. Kikubwa tumuombe huko aliko mungu ampunguzie adhabu ya kaburi,”amesema Sheikh Kalokola.

Hayati Dk John Magufuli enzi za uhai wake

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga alisema Hayati Rais Magufuli alijipambanua kuwa mtetezi wa wanyonge na kwamba ni vema Watanzania wakaendelea kunuenzi na kumkumbuka kwa mema aliyoyafanya.

Ibada hiyo maalum ilifanyika katika Viwanja vya CCM Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu Na kwamba iliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi.

Aidha, Viongozi wa dini wakiwemo wa Kanisa Katoriki, KKKT, Kanisa la Halisi la Mungu Baba, Kanisa la Wasabato.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles