29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia aongoza Maelfu ya waombolezaji kumuaga Dk. Magufuli Dar

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Machi 20, 2021 ameongoza maelfu ya wananchi katika Mkoa wa Dar es Salaam kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dk.John Magufuli, ambaye ameagwa leo Machi 20,2021 katika Uwanja wa Uhuru.

Dk. Magufuli alifariki dunia Machi 17,2021 katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo na leo kwa mujibu wa ratiba wananchi wa mkoa huo wakiongzwa na Rais Samia wametoa heshima za mwisho kwa mwanamapinduzi na mpenda maendeleo wa Taifa la Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho na kuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dk.John Magufuli ambaye ameagwa leo Machi 20,2021 katika Uwanja wa Uhuru Mkoa wa Dar es Salaam.

Kabla ya Rais Samia kuongoza kutoa heshima za mwisho ilifanyika Misa maalum katika Uwanja huo wa Uhuru iliyoanza baada ya mwili kuwasili saa 10:13 asubuhi ukitokea Kanisa la mtakatifu Petro (St.Peters’) ambako nako ilifanyika Misa ya wafu.

Baada ya Rais Samia kutoa heshima zake kwa Dk.Magufuli alifuata Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa amefuatana na mkewe Mary Majaliwa na baada ya Waziri Mkuu kutoa heshima zake aliondoka uwanjani hapo.

Wengine walitoa heshima ni Mama Maria Nyerere, akifuatiwa na Mama Janeth Magufuli aliyeongozona na familia yake, Viongozi wengine ambao waliotoa heshima za mwisho ni Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Bashiru Ally Kakulwa.

Wengine ni Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abedi Karume, majaji wastaafu wakiwamo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalaama, pia viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo Mawaziri pamoja na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baadaye wakafuata wananchi waliokuwa wamesimama katika misururu mirefu.

Askari wa Jeshi la Wananchi wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Hayati Dk. John Magufuli

Awali wakati akiongoza Misa katika Uwanja huo, Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Tadeus Rweich amewaomba watanzania waliojitokeza viwanjani hapo na waliotazama kupitia televisheni zao majumbani, amumelezea Hayati Dkt. Magufuli ambapo amesema alikuwa ni Rais aliyeipenda nchi yake na alifanya kazi zake kwa uzalendo mkubwa na kwa nguvu zake zote.

Askofu Rweich amesema Dk.Magufuli alikuwa ni mtu wa Mungu kweli kwani kila alichokifanya kwake Mungu alikuwa mbele, huku akiongeza kuwa alijali maslahi ya Taifa na aliwapenda Watanzania kwa vitendo.

Aidha, Askofu Rwaich ametoa pole kwa Rais Samia pamoja na familia ya Hayati Dk.Magufuli, Mama Janeth Magufuli katika kipindi hiki kigumu huku akimsihi kuwa mstamilivu na kushikamana na Mungu na kubwa zaidi kumuombea.

Pia ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa Watanzania wote na kuwataka kujipa moyo na matumaini na kwamba yeye hana shaka kwamba Rais Samia atatenda vyema, haki katika shughuli zake mpya majukumu yake.

Aidha, kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa mapema leo, siku ya kesho Jumapili Machi 21, Wakazi wa Dar es Salaam watapata fursa nyingine ya kumuaga Hayati Dk. Magufuli katika uwanja huo wa Uhuru kabla ya mwili wake kupelekwa jijini Dodoma siku ya Jumatatu.

Sambamba na utaratibu huo pia kumekuwapo na mabadiliko ya ratiba ambapo sasa siku ya Jumanne ataagwa na wakaazi wa Jiji la Zanzibar kabla ya kupelekwa Jijini Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles