24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Simanzi, Vilio vyatawala Rais Samia akiongoza viongozi kumuaga Magufuli

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Vilio na simanzi vimeendelea kutawala kwa maelefu ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na viongozi wastaafu wa serikali zilizopita wamefika Uwanja wa Uhuru kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Magufuli.

Dk.Magufuli ambaye amefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mnzena mkoani Dar es Salaam ambako alikuwa anapatiwa matibabu kutoka na maradhi ya moyo katika mfumo wa umeme, wananchi wa Dar es Salaam wakiongozwa na maelfu ya wananchi wamepata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kwa Dk.Magufuli.

Uwanja wa Uhuru ambao siku zote umekuwa maarufu kwa kutumika katika matukio makubwa ya kitaifa ikiwa mo pia shughuli mbalimbali za kimichezo na burudani kwa leo umekuwa ni sehemu ya majonzi kwa Watanzania wakimuaga aliyekuwa rais wao Dk. John Magufuli.

Uwanjani hapo maelfu ya wananchi walianza kujitokeza mapema alfajiri ya leo Machi 20, 2021 ambao waliokuwa wametoka maeneo mbalimbali na wote wakiwa na hamu ya kushuhudia shughuli mbalimbali za kutoa heshima zao za mwisho kwa Dk.Magufuli ambaye kwenye uongozi wake aliamini katika kuwasadia na kusikiliza wananchi wanyonge wenye changamoto mbalimbali za kimaisha.

Mwili wa Dk.Magufuli ulifikishwa Uwanja wa Uhuru saa nne asubuhi ukitokea Kanisa la St.Peters, Dar es Salaam ambako ibada maalum ya kumuaga ilifanyika kabla ya wananchi na viongozi kutoa heshima zao za mwisho katika uwanja huo.

Hata hivyo kote ambako mwili wa Dkt.Magufuli umepitishwa maelfu ya wananchi walikuwa barabarani.Wananchi walishindwa kabisa kuwa na ustahimilivu kwani asilimia kubwa ya wananchi hao walionekana wakibubujikwa na machozi kutokana na mapenzi makubwa waliyokuwa wanayo kwa Dkt.Magufuli ambaye kwenye utawala wake alihakikisha awatetea na kuwapigania.

Pamoja na hayo kabla ya wananchi wakiongozwa na viongozi kuanza kutoa heshima zao za mwisho ibada maalum ilifanyika uwanjani hapo na wakati wa ibada hiyo mengi yamezungumzwa kuhusu Dk.Magufuli.

http://www.mtanzania.co.tz inaendelea kukulwta matukio mbalimbali yanayaojiri juuu ya msima huu mzito

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles