28.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa Dini Musoma waeleza juhudi zinazofanywa na Jeshi la Polisi kulinda amani

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Viongozi mbalimbali wa dini mkoani Mara wamelaani vitendo vya uhalifu mkoani humo na kulitaka Jeshi la Polisi kusimamia usalama wa raia na mali zao kwa njia zote madhubuti.

Hayo yamesemwa hii Septemba 28, 2022 mjini Musoma na Viongozi wa dini za Kiislam pamoja na kikristo ambapo wametumia muda huo kueleza namna wanavyotumia nyumba za ibada kuhubiri amani na kulinda amani ya kila raia nchini.

Pia, viongozi hao wametanabaisha kuwa matumizi yoyote ya silaha za moto kwa Jeshi la Polisi ni sahihi tu pale ambapo uhalifu unaokabiliana nao unalazima matumizi ya bunduki na risasi.

Kauli hii ya viongozi wa dini inakuja mata tu baada ya Jeshi la Polisi kufanikiwa kuwadhibiti wahalifu wawili hivi karibuni mkoani Mara ambapo katika majibizano ya risasi na watu hao wanaosemekana kuwa majambazi na kukutwa na silaha za moto, wahalifu hao walipoteza maisha katika mapambano na jeshi la polisi.

“Matumizi ya silaha yanalazimu pale tu ambapo vijana hawa ambao kimsingi hawana amani mioyoni mwao, na pia hata familia zao na malezi yao hayakuwa na amani, hivyo wanapotumia silaha inaweza kulazimu askari kutumia silaha pia,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles