27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa dini ‘kurudishwa’ darasani

*Lengo ni kudhibiti vitendo vya ukatili

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Viongozi wa Dini nchini ambao wamekuwa wakitumika kuwafundisha watoto maadili ya dini watalazimika kufundishwa tena maadili ya dini ili kusaida kupunguza vitendo vya ukatili.

Aidha, kutokuwa na misingi bora ya dini kwa walimu wengi tangu wakiwa wadongo ndiyo chanzo pia cha kukithiri kwa vitendo vya ukatili katika jamii.

Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo Jumatano Oktoba 12, 2022 na Mwenyekiti wa Islamic Education Panel(IEP), Mohamed Kassim wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa elimu ya dini kiislamu darasa la saba uliofanyika Septemba, mwaka huu.

“Viongozi wa dini wanabaki kuwa wanaadamu kama walivyo wengine na wanaweza kukosa kama ilivyo kwa wengine pia wanaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa makosa kama wanavyochukuwa wanadamu wengine isipokuwa tu ni jambo la kusikitisha kwa mtu ambaye ulimtegemea ndiye awe mwalimu wa kusimamia maadili yeye akakosa maadili hayo au akwa msimamizi mbaya wa maadili hayo.

“Kama viongozi wa dini hilo tumeliona na tumeliingiza katika vikao vyetu mbalimbali kwani kama tunavyoona wapo viongozi wa dini wa kiislamu na wa madhehebu mengine. Tunayo makundi yanayotuunganisha viongozi wa dini ambapo tumeanza kufanya vikao ili kufanya kila watu katika eneo lao kuweza kushughulika na ukosefu wa maadili wa watendaji na viongozi wa dini kwenye eneo lao.

“Tunahitaji kufanya semina elekezi kwa viongozi wetu na walimu wetu juu ya dhaha hii ya maadili na mambo mengi yanayokuja sasa, kuna mambo ya ukatili, ulawiti haya yanatokea kwa hiyo tumepewa kazi ya kutoa semina elekezi kwa viongozi wetu wa dini, shuleni, madrasa na maimamu ili kulizungumzia pamoja hili kwani tunaamini kwa kufanya hivyo kutasaidia kuwakumbusha kwani binadamu anatabia ya kujisahau,” amesema Kassim.

Amesema wao kama waislamu watakaa lakini pia wanaunganisha nguvu pamoja na viongozi wengine ili kudhibiti vityendo vya ukatili.

“Kwa hiyo sisi waislamu tutakaa lakini pia tunaunganisha nguvu zetu pamoja na viongozi wa madhehebu mengine katika kuhakikisha kwamba tunadhibiti tatizo hili lililojitokeza.

“Lakini wakati mwingine tatizo hili linaweza kusababishwa na mifumo yetu au sera za kikazi ambazo zinamtaka mtu asiolewe wala asioe, hivyo kila mmoja anatakiwa kuangalia upande wake ili viongozi wa dini wawe mfano wa kuigwa,” amesema Kassim.

Awali, akizungumzia matokeo hayo amesema kuwa Jumla ya shule 3, 710 katika mikoa 25 na Halmashauri 151 zilishiriki kufanya mtihani huo.

“Watainiwa waliosajiliwa walikuwa 163,143 na waliofanya mtihani walikuwa 142,522 sawa na asilimia 87.36 huku watainiwa 20,621 wakishindwa kufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali.

“Idadi ya ya watainiwa waliofaulu kwa kupata madaraja A hadi C ni 95,166 sawa na asilimia 66.77 ya watainiwa wote. Aidha, watainiwa waliopata daraja D na E ni 47,356 sawa na asilimia 33.23 ya watainiwa wote,” amesema Kassim.

Upande wake Amir Mkuu Baraza Kuu la Jumhiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mussa Yussufu Kundecha alisema wanafunzi 3,567 wamefanya vizuri kwa kupata ufaulu wa alama A katika mtihani huo nakwamba ufaulu huo umeenda vizuri ikilinganishwa na mwaka jana.

“Shule 10 bora kwa kitaifa katika kundi la shule zenye watainiwa 20 au zaidi namba moja ni Mumtaaz ya Mwanza, Istiqaama ya Tabora, Rahma ya Dodoma, Algebra Islamic ya Dar es Salaam, Dumila ya Morogoro, Islamia ya Mwanza, Hedaru ya Kilimanjaro, Daarul Arqam, Mbagala Islamic na Maarifa Islamic zote za Dar es Salam.” amesema Sheikh Kundecha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles