22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Maandalizi ya kuhitimisha mbio za mwenge yakamilika Kagera

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako amesema maandalizi ya kuhitimisha mbio za mwenge Oktoba 14, mwaka huu yamekamilika.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo Oktoba 12, 2022 wakati wa ukaguzi wa maandalizi hayo katika viwanja vya Kaitaba, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambapo mbio za mwenge wa uHuru zitahitimishwa Kitaifa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema amekagua na kuridhika na maandalizi hayo ikiwemo halaiki ya watoto na vikundi mbalimbali vya michezo na hivyo kutumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kujitokeza katika kilele cha mbio za mwenge.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) – Zanzibar, Hamza Hassan Juma amesema mwenge huo umepita Mikoa yote ya Tanzania wakuu wa mikoa wote wanashirikiana na wakuu wa Wilaya.

“Kama mwenge unavyoleta matumaini tuendelee kuwapa tumaini vijana na kushikamana kila pahala ili kudumisha amani yetu,” amesema Waziri huyo.

Amesema Watanzania wataendelea kuziunga mkono mbio za mwenge wa uhuru ili vizazi vinavyokuja viendelee kuuenzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albart Chalamila amewataka wananchi kutumia ugeni huo kutoa huduma nzuri za malazi na chakula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles