30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi Afrika pasua kichwa

Thabo Mbeki
Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki

NA EVANS MAGEGE, Dar es Salaam

VIONGOZI wa Afrika wameelezwa  si wasimamizi wazuri wa maendeleo  ya watu wao jambo ambalo limesababisha bara hilo kuendelea kuwa masikini na tegemezi kwa mataifa makubwa.

Hayo yalielezwa na baadhi ya marais wastaafu katika, wasomi na viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Dar es Salaam jana, kwenye mkutano kuhusu jinsi ya kuliondoa bara hilo katika dimbwi la umaskini na unyonge.

Katika mkutano huo wa siku mbili, baadhi ya washiriki   walionyesha wasiwasi  kuhusu jinsi viongozi katika bara hilo   wanavyosimamia rasilimali za nchi zao, ingawa wana mvuto wa siasa.

Mkutano huo uliodhaminiwa na taasisi mbalimbali, umeandaliwa na Taasisi ya Uongozi Dar es Salaam inayoongozwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Akijibu   maswali ambayo pamoja na mambo mengine yalilenga mienendo ya viongozi wa Afrika kama wanaweza kuleta mabadiliako yanayotarajiwa, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, alisema kuna wasiwasi mkubwa  kuhusu   viongozi wa Afrika kama wanaweza kuzikwamua nchi zao kwenye umaskini na unyonge.

“ Kuhusu ubora wa viongozi …sijui nitumie lugha gani ya kidiplomasia.  Kuna wasiwasi mkubwa… hata mimi nina wasiwasi na aina ya viongozi tulionao katika siasa na hata  biashara.

“Kama wangekuwa na mfumo mzuri wa mawasiliano kati yao na wananchi  ungekuwa   msingi bora wa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya waafrika,” alisema Mbeki.

Alisema  kiongozi bora ni yule anayeimarisha mawasiliano yake na wananchi kwa lengo ya kuongoza na kusimamia yale yanayotakiwa na wananchi ili kwa pamoja waweze kujenga uchumi wenye kuwaletea maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles