23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi ACT Wazalendo ziarani Pemba

Na Mwandishi Wetu, Pemba

Viongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, wakiongozwa na  Kiongozi wao,Zitto Kabwe, leo Agosti 9, 2021 wameanza ziara ziara ya siku mbili kwenye mikoa ya Kichama Pemba.

Wengine ni Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Juma Duni Haji, Katibu Mkuu Ado Shaibu na Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman.

Akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha ziara hiyo kilichofanyika katika Jimbo la Konde na kuhudhuriwa na viongozi wa Mkoa, Majimbo na Matawi  ya Mkoa wa Kichama wa Micheweni, Ado Shaibu ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuwaeleza viongozi na wanachama wa ACT maazimio ya kikao cha dharura cha Kamati Kuu kilichofanyika Unguja jana kilichoitishwa kufuatia hujuma iliyofanyika katika uchaguzi wa marudio Jimbo la Konde.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo, Salim Bimani, katika kikao hicho viongozi waliwasilisha maazimio ya Kamati Kuu wakisisitiza umuhimu wa mazungumzo katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Makamu wa Kwanza wa Rais Masoud, ameeleza kuwa kabla na baada ya uchaguzi wa marudio katika jimbo la Konde, yeye na viongozi wengine wa chama walifanya jitihada na kuchukua hatua mbalimbali kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Hussein  Ali Mwinyi kutatua kadhia ya jimbo hilo.

Amesema kutokana na jitihada hizo za pande zote mbili, ndio sababu ya mgombea wa CCM aliyetangazwa kuwa mshindi kinyume na matokeo halisi ya uchaguzi huo alijiuzulu.

Amewaeleza viongozi wa Mkoa wa Kichama wa Micheweni kuwa Kamati Kuu imepongeza hatua hiyo ya mazungumzo na kutoa rai kuwa itumike pia katika kushughulikia masuala mengine makubwa yanayoikabili Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wake.

Naye Makamo Mwenyekiti Zanzibar Duni Haji, aliweka bayana kuwa ingawa chama kimeridhia kushiriki katika  uchaguzi wa marudio, ni lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe.

Amesema ni lazima wasimamizi na wasaidizi wa uchaguzi waliosimamia katika Jimbo la Konde wasirejeshwe tena kusimamia uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ndani ya Serikali wawajibishwe.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Cham, Zitto, ameweka bayana kuwa mbali na matakwa ya kikatiba, ACT Wazalendo kiliingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kutokana na makubaliano yaliyotokana na mazungumzo baina ya Mwenyekiti wa Chama Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad na Rais Mwinyi.

Akiyataja makubaliano Zitto  amesema  moja wapo ni Maalim Seif na Rais Mwinyi walikubaliana kuachiwa huru kwa viongozi na wanachama wote wa upinzani wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na kesi za kisiasa zilizotokana na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020

Zito ameongeza kuwa Kamati Kuu imeazimia kuwa na wawakilishi ndani ya Serikali wakiongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais ili kushirikiana na viongozi wa chama kufuatilia utekelezaji wa makubaliano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles