23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mashabiki wa ngumi Moro wamtahadharisha Dulla Mbabe

Na Ashura Kazinja, Morogoro.

MASHABIKI wa mchezo wa ngumi mkoani Morogoro wamemtahadharisha bondia  Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’, kujiandaa  na kipigo kutoka kwa Twaha Kiduku katika pambano lao la kushindania gari litakalofanyika  Agosti 20, 2021 jijini Dar es Salaam.

 Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau hao akiwamo Nestory Alexander, wamesema mchezo wa ngumi ni mchezo ambao unahitaji nidhamu na kumsikiliza mwalimu mambo ambayo Kiduku anayo na yatamfanya  abebe gari hiyo.

Alexander amesema Kiduku atampa kipigo Dulla kutokana na  mazoezi  anayofanya kwenye maeneo yenye milima  tofauti na mpinzani wake.

Naye Godfrey Kasambula amesema anaamini kwa asilimia 100 kuwa Kiduku atashinda katika mpambano huo akiamini ni bondia mzuri na mwenye uwezo mkubwa aliounesha tangu kwenye mapambano ya mwanzo, ambapo katika pambano la kwanza walitoka sare, la pili Kiduku alishinda.

Aidha Twaha kiduku akizungumzia mchezo huo amewashukuru wadhamini  kwa kuona umuhimu wa kuwashindanisha mara ya tatu ikionesha  kuaminiwa na wadhamini mara kwa mara, hivyo  atahakikisha anarudisha ushindi Morogoro.

Naye muandaaji  wa pambano hilo, Kapteni Suleiman Semunyu, amesema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba wataanza na mapambano ya utangulizi kutoka kwa mabondia tofauti wa ndani ya Morogoro mapambano yatakayofanyika Agosti 14 kwenye ukumbi wa FZ Florida- Msamvu na kuwaomba wadau wa ngumi kujitokeza kwa wingi kupata burudani hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles