31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mulamula amuaga Balozi wa Oman

Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, amemuaga Balozi wa Oman nchini, Ally Abdallah Almahruqi ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi.

Balozi Mulamula amempongeza Almahruqi kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Oman na Tanzania wakati wote wa uwakilishi wake hapa nchini.

“Tanzania tunashukuru zaidi kwa ushirikiano uliotuonesha wakati wote ulipokuwa hapa kama Balozi na tunakuahidi kuudumisha na kuuendeleza ushirikiano huo kwa maslahi ya nchi zetu mbili,”amesema Balozi Mulamula

Kwa upande wake Balozi Almahruqi ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano alioupata wakati wote alipokuwa akitekeleza majukumu yake.

“Nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipatia wakati wote niliokuwa hapa nikitekeleza majukumu yangu kama Balozi, hakika nilifarijika sana, naahidi kuwa nitakuwa balozi mwema kwa Serikali ya Tanzania,” amesema.

Pia Balozi ameipongeza Tanzania kwa hatua inazochukua za kupambana na virusi vya Corona ikiwamo kuungana na mataifa mengine duniani kuchanja chanjo ya UVIKO-19.

Tanzania na Oman zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali ikiwamo uwekezaji katika madini, mafuta, gesi, kilimo, usafirishaji, utalii na biashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles