27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Viongozi 500 wa Serikali kuhakikiwa mali zao

Anjela Kairuki
Anjela Kairuki

GRACE SHITUNDU Na ELIAS SIMON ( TUDARCO)

SEKRETERIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inatarajia kuanza uhakiki wa mali za viongozi wapya 500 walioingia serikalini, huku onyo likitolewa kwa watakaokuwa wametoa taarifa za uongo.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora),  Anjela Kairuki, baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau  ambao walikuwa wakijadili rasimu ya taarifa ya utafiti wa hali ya maadili nchini.

Alisema  kwa mwaka huu viongozi wa umma wameongezeka tofauti na miaka ya nyuma, ambapo walikuwa wakifanya uhakiki wa mali za viongozi 100 hadi 200 tu kwa mwaka .

“Pamoja na uhakiki kufanyika tunaomba wananchi wajitokeze kwenda kukagua daftari lile lenye matamko ya mali na madeni ili kuweza kujua zaidi kila ambacho kiongozi amekiandika katika tamko ndicho anachokimiliki na endapo itaonekana sivyo watoe taarifa kwa Sekreterieti.

“Hiyo itaweza kuzidisha wigo  na kurahisisha wakati wa kwenda kufanya uhakiki  hali inayoweza kufanya uhakiki wa viongozi hadi 1000,” alisema Waziri Kairuki.

Akizungumzia viongozi  wa umma ambao hawarejeshi fomu za mali na madeni kwa wakati, alisema atakayekiuka sheria hiyo hatofumbiwa macho.

Kuhusu ripoti iliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma, Waziri Kairuki alisema takwimu zinaonyesha katika tafiti ndogo zinatofautiana kutokana na wigo wa watu waliohojiwa na uelewa wao.

Awali akiwasilisha taarifa Katibu wa Sekreterieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu Salome Kaganda, alisema utafiti uliofanywa mwaka 2014 unaonyesha asilimia 95.2 ya viongozi wa umma wanatambua uwepo wa sheria ya maadili ya viongozi umma.

“Asilimia 53 waliisoma sheria  huku 35 wanafahamu uwepo wa utaratibu wa kuwasilisha malalamiko na asilimi 63 wanaogopa kutoa taarifa za watumishi wenzao pale wanapoikuka maadili,” alisema Jaji Kaganda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles