24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Ufisadi wa kutisha watikisa Mbeya

Amos Makalla
Amos Makalla

Na Pendo Fundisha, Mbeya

ZAIDI ya Sh milioni 190 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ulipaji wa fidia wananchi wa vijiji 21 wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya, zinadaiwa kutafunwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo.

Fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya kulipa fidia wananchi hao ili wahame kupisha Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambazo zilitakiwa kulipwa pamoja na kujenga shule ya msingi na zahanati ya ya Kijiji cha Ikoga Mpya.

Kutokana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG), alibaini fedha hizo kupotea huku wananchi wa vijiji 21 wakiwa hawajalipwa fidia hiyo.

Hali  hiyo ilimfanya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, akuingilia kati na kuhoji waliohusikana na ubadhirifu huo.

“Ulipwaji wa  fedha hizi ulighubikwa na udanganyifu mkubwa, taarifa ya CAG imetoka katika ulipaji wa fidia kiasi cha shilingi milioni 192 zimeliwa na wajanja,”alisem Makalla  alipokuwa akizungumza na wanakijiji wa Ikoga Mpya.

Alisema CAG amebaini kuwapo kwa baadhi ya watu  ambao hawakufanyiwa tathmini lakini walilipwa fedha huku taasisi kama shule, zahanati na msikiti fedha zao zikitafunwa na wajanja wachahe.

“Mtu hayupo eneo la tukio lakini kaandikwa jina kachukua shilingi milioni 26, anaitwa Twaha Mlidi Jemedali anatoka Kijiji cha Upagama Kitongoji cha Mbuyuni, yeye ana duka la dawa.

“Alikuwa mfanyabiashara akajiingiza na kulipwa, pili shilingi milioni 156 zilitolewa kwa ajili ya kujenga shule, zahanati lakini zimeliwa lakini kubwa zaidi ni pale watu wamediliki hata kula fedha za ujenzi wa Msikiti wa Msangaji shilingi milioni 9,” alisema.

Kutokana na hali hiyo Makalla, alisema kuwa watendaji waliohusika ni lazima wasakwe na wachukuliwe hatuaza kisheria licha ya kuhamishiwa kwenye maeneo mengine.

“Lazima hawa wachukuliwe hatua kali za kisheria pamoja na kuzirejesha fedha hizi, hata kama mtu huyo atakuwa Manyara au Musoma aitwe ili haje kujibu mashtaka haya,” alisema Makalla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles