28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Vilabu vya uhamasishaji vinavyochangia uelewa wa sheria

Janeth Mushi, Arusha

Vilabu vya uhamasishaji wa haki ardhi katika shule za sekondari za kata vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha, vinatajwa kuongeza uelewa wa jamii juu ya umiliki wa ardhi na mali kwa wanawake na kupunguza migogoro ya ardhi.

Vilabu hivyo 10 vilivyoanzishwa mwishoni mwa mwaka jana na Chama cha Wanasheria Wanawake (Tawla), tawi la Arusha, vinatekelezwa chini ya mradi wa ukuzaji haki ya upatikanaji wa ardhi na mali kwa wanawake unaofadhiliwa na Shirika la Foundation For Civil Society.

Akizungumza juzi wakati wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa kabu hiyo ya haki ardhi, mmoja wa wanachama wa klabu hiyo katika Shule ya Sekondari Kitefu, ambayo ni moja ya shule inayotekeleza mradi huo, Halima Ally, amesema kuwa upo umuhimu mkubwa wa elimu hiyo kuendelea kutolewa katika makundi mbalimbali ya jamii.

Amesema kuwa elimu hiyo itawezesha wanawake kupata haki ya kumiliki mali ikiwa ni pamoja na ardhi sambamba na kupunguza migogoro ya ardhi katika jamii ambayo kwa kiasi kikubwa inachangiwa na kukosekana kwa elimu hiyo muhimu huku jamii ikimtenga mwanamke katika suala la umiliki tofauti na mwanaume.

“Elimu hii itasaidia kuelimisha makundi mbalimbali juu ya haki sawa kwa wote, sisi hapa shuleni tunakutana kila jumatano na kuelimishana juu ya masuala ya haki ardhi baada ya kupewa elimu hii ambayo ni muhimu kwani sisi ni watoto wa wakulima na wafugaji,hivyo  tunaenda kuwa mabalozi wazuri majumbani kwetu na itatusaidia kupunguza migogoro ya ardhi,” amesema.

Awali Mwanasheria wa Tawla, Sylvia Mwanga, ambaye pia ni  Mtekelezaji wa mradi huo, amesema lengo la kuanzisha vilabu hizo ni kuongeza uelewa wa jamii kuondokana na mila na desturi potofu zilizokuwa zikizuia umiliki wa mali na ardhi kwa wanawake na kuwa wameanza kutembelea shule hizo kuona namna wanaendesha vilabu hivyo ili kuona iwapo lengo la kuanzishwa kwake linafikiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles