23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Miili ajali Tarime kuzikwa, kutambuliwa kwa DNA

TIMOTHY ITEMBE-TARIME



MKUU wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, amesema   marehemu  15 waliofariki dunia katika ajali ya gari mbili za abiria zilizogongana na kuwaka moto   watazikwa eneo la ajali.

Amesema miili hiyo itachukuliwa sampuli za vipimo vinasaba (DNA)  i watakapojitokeza ndugu iweze kutambuliwa.

Akizungumza  mjini hapa jana, Malima alisema   miili hiyo  imeharibika kutokana na kuungua kwa moto na upo uwezekano wa baadhi ya ndugu kushindwa kuitambua vema miili ya wapendwa wao lakini wataweza kuitambua  kwa njia ya DNA.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Tarime na Rorya, Henry Mwaibambe, alisema ajali hiyo ambayo ilitokea juzi saa 9  alasiri katika barabara ya Tarime-Musoma   Kijiji cha Komaswa, ilisababisha vifo vya watu 15 na wengine wanne kujeruhiwa.

Alisema mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika lakini wakati magari hayo yakigongana kulikuwa na mvua kubwa iliyokuwa imeambatana na upepo mkali na baadaye kukatika.

Kamkanda alisema ajali hiyo ilihusisha  gari la abiria   la Mazda Bongo lililokuwa   likiendeshwa na Jossephat Amon (39) mkazi wa Kigera Musoma likitokea Musoma kwenda Tarime Mjini lililogongana uso kwa uso na gari nyingine la Toyota Hiace   lililokuwa likitoka Tarime Mjini kwenda Ruhu Kinesi likiwa linaendeshwa na Chacha Marwa (45) mkazi wa Nyamaguku.

Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Thomas Josephat (24) aliyevunjika mguu wa kulia ambaye alikuwa kondakta wa Mazda Bongo na mtoto wa dereva wa gari hiyo,   Blandina Machage (24) mkazi wa Wegero ambaye amevunjika mguu wa kushoto.

Wengine ni Rhobi Kiginga (36), ambaye ameungua na moto mwili mzima na kuvunjika mguu wa kulia   na Leonard Mweko (37), mkazi wa Kinesi ambaye ameungua sehemu mbalimbali za mwili wake na kuvunjika mguu wa kulia pia.

“Majeruhi wote walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya Tarime kwa matibabu na kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Bugando  Mwanza kwa ajili ya matibabu zaidi.

“Miili ya waliofariki dunia  imeungua sana na haijatambuliwa, imepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hospitalini Tarime kwa ajili ya utambuzi na uchunguzi wa utabibu kisha kukabidhiwa kwa maziko kwa wahusika,” alisema.

Utaratibu huo wa kutumia DNA ulianza kutumiwa wilayani Ukerewe Mkoa wa Mwanza katika Kisiwa cha Ukara baada ya Kivuko cha MV Nyerere kuzama   ndani ya Ziwa Victoria Septemba 20, mwaka huu eneo la Bwisya na kusababisha vifo vya watu vya watu 120.

Utaratibu huo uliwezesha kutambuliwa   mwili mmoja ambao licha ya kuharibika, ndugu zake walipimwa DNA na kufananisha na zile za maiti walizozika hivyo kuonyeshwa kaburi la ndugu yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles