23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana watakiwa kununua nyumba

Na Mwandishi Wetu

VIJANA wametakiwa kujifunza kununua nyumba badala ya kutunza fedha kujengakwa kuwa sehemu nyingi duniani watu hawajengi nyumba bali wananunua.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa kusherehekea miaka miwili ya jengo la Palm Village usiku wa kuamkia leo, jijini Dar es Salaam.

“Mpango wa kununua nyumba, umeanza muda mrefu, watu wanaweza kudhani Dar es Salaam imejaa lakini hawajui wanaweza kununua nyumba hata Masaki nyumba zipo zimejengwa kwa ajili ya kuuzwa na ukinunua unapata hati yako.

“Tunasheria ya umirikishaji wa ardhi na tunasheria ya mabenki ya kukopesha fedha, kwa kuanzia serikali kupitia benki kuu imetoa zaidi ya shilingi bilioni 400 kupeleka kwenye mabenki kukopesha wananchi kwa gharama nafuu waweze kuleta maendeleo.”

“Vijana ni wakati wa kununua nyumba na kumiliki hati yako, ukiwa na mradi wa hata dora 100 ukitaka kumilikishwa ardhi utamilikishwa ili uweze kuleta maendeleo kwa Watanzani.”

Aidha aliongeza kuwa Kigamboni kuna viwanja zaidi ya elfu kumi ambavyo vimepangwa na kupimwa itakusaidia kutopata usumbufu wa migogoro ya ardhi.

Mkurugenzi  wa Palm Village, Jansen  Palm,  amefurahi kwa kutimiza miaka miwili na kuwataka watu wazidi kujitokeza katika kununua na kupanga

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles