28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana Siha watakiwa kuchangamkia fursa

Na Allan Vicent, 

Vijana wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuchangamkia fursa za ajira zilizoko kwenye sekta ya utalii kwa kujiunga na vyama vya waongoza watalii au wabeba mizigo ya watalii (wapagazi) ili kujipatia kipato.

Ushauri huo umetolewa juzi na Mkuu wa Wilaya hiyo Onesmo Buswelu alipokuwa akizungumza wadau mbalimbali wa utalii wakiwemo waandaaji wa mbio za Siha Afya Marathon.

Alisema kuwa utalii ni miongoni mwa sekta zenye fursa za ajira lakini vijana wengi wamekuwa wakikaa vijiweni na kulalamika kukosa ajira badala ya kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiunga na wenzao wanaofanya shughuli hizo.

Alibainisha kuwa kuongoza watalii ni fursa nzuri ya ajira kwa vijana ikiwemo ya upagazi (kubeba mizigo ya watalii), hivyo akawataka kuchangamkia fursa hiyo ili kujipatia kipato.

‘Sekta ya Utalii ina fursa nyingi za ajira, vijana changamkieni fursa fursa hizo, watalii wanaokuja kupanda Mlima Kilimanjaro wengine wanapitia lango la Lemosho na Londros lililopo hapa Siha, lakini waongozaji ni wachache’, alisema.

 Buswelu alisisitiza kuwa fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hii zinawafaa sana vijana hivyo akawataka kutokaa vijiweni au kushinda wakicheza ‘pool table’ na kulalamikia kuwa hawana ajira wakati fursa zinawasubiri.

Aliwataka wale wote wasio na ajira kujisajili ili wapewe utaratibu wa namna ya kuongoza au kupandisha watalii katika Mlima Kilimajaro na maeneo mengine.

“Huu ni wakati wa vijana wa Siha na maeneo mengine hapa nchini kutambua fursa zilizopo katika sekta hii na kuzitumia ili kujipatia kipato na kusaidia familia zao ikiwemo kujenga uchumi wa taifa,” alisema.

Daktari Mkuu wa Magonjwa ya Kifua Kikuu (TB), Riziki Kisonga kutoka Hospitali Kuu ya Kifua Kikuu ya Kibong’oto aliwataka vijana kuchangamkia fursa za upandaji Mlima Kilimanjaro kwa kuwa kupanda mlima ni zoezi tosha na kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo Kifua Kikuu.

Aliwataka wakazi wawilaya hiyo kuendelea kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambikizwa na yanayoambukizwa ikiwemo kifua kikuu (TB) kwani kila saa watu 74 hufariki kutokana na TB.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles