Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Rehema Nchimbi (kulia) akikabidhi vikundi vya kainamama na vijana mfano wa hundi ya sh milioni 91 zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida kwa ajili ya vikundi vya Akinamama,vijana na wenye ulemavu ,makabidhiano hayo yalifanyika jana kwenye Ofisi za Halmashauri hiyo,kushoto kabisa ni Mbunge wa Jimbo Iramba Mashariki, Francis Isack.
Meneja Mahusino Serikalini Benki ya NMB Kanda ya Kati, Peter Masawe (kushoto) akimkabidhi msaada wa madawati Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Rehema Nchimbi (wapili kulia), NMB ilikabidhi madawati 100 kwa ajili ya shule mbili za Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida wenye thamani ya sh milioni 10, shule hizo ni shule ya Msingi na Ndala, kulia kabisa ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Jackson MasakaÂ