23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yawazawadia washindi 12 zawadi mbalimbli

Na Mwandishi Wetu

Benki ya NMB imewazawadia washindi 12 zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya milioni 28 kwenye bahati nasibu ya mwezi wa 12.

NMB kupitia kampeni yake ya ‘MastaBata siyo Kikawaida’ imewazawadia washindi hao zawadi ikiwamo simu janja, Runinga za kisasa, na Jokofu ambapo kila msindi alipatiwa zawadi zenye thamani ya shilingi Milioni 2.4 kila mmoja.

Akizungumza wakati wa kuwatangaza washindi, Maneja wa Benki hiyo tawi la Mlima City, Ireen Masaki alisema dhumuni la kampeni hiyo ni kuwahamasisha wateja kutumia kadi za Mastercard kufanya manunuzi ya bidhaa au huduma kupitia mtandaoni.

Miongoni mwa wateja walioshinda zawadi hizo ni Happy Luka Pallangyo, Masunga Jasila, Francis Julian na Rose Marealle. Mchakato wa kuwapata washindi hao ulisimamiwa na Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kuhahatisha Tanzania.

Promosheni hiyo ilizinduliwa Novemba, mwaka huu na Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara NMB, Filbert Mponzi, na itamalizika Februari, mwakani.

Akizindua promosheni hiyo, Mponzi alisema NMB inahamasisha na kutoa fursa ya kipekee kwa wateja kufurahia huduma zinazotolewa na benki hiyo.

Alisema kampeni hiyo itakuwa na droo za kila wiki na kila mwezi. Wateja wanapaswa kufanya miamala yao kupitia kadi ya NMB Mastercard au QR mara nyingi kwa kuwa kila unapofanya muamala unaongeza nafasi moja ya kushinda.

Alisema katika kipindi chote cha kampeni, NMB itakabidhi zawadi kwa washindi 40 watakaoshinda Sh. 100,000 kila wiki na washindi 12 watazawadiwa simu janja aina ya Samsung galaxy Note20 yenye thamani ya  Sh. milioni 2.48 kila mwezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles