23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

VIGOGO WATATU WA ACT MANYARA WAJIUZULU

Na BEATRICE MOSSES, Babati

VIONGOZI watatu wa Chama cha Alliance for Change and Transpancy (ACT) Wazalendo Mkoa wa Manyara wamejiuzulu nafasi zao.

Vilevile wamejitoa uwanachama wakidai uelekeo wa chama hicho  si mzuri.

Walisema  wamefikia uwamuzi huo baada ya kuona mwenyekiti na katibu wa chama hawaelewani.

Katibu wa Ngome ya Wazee ACT Mkoa wa Manyara, James Lolottu, alisema  a hivi karibuni kulikuwa na mgogoro kati ya katibu wa   mkoa wa chama hicho na mwenyekit wake.

“Tumepata matatizo  hapa katikati, kama katiba ya ACT Wazalendo inavoeleza.

“Anayehusika  kuitisha vikao  vya chama ngazi ya mkoa ni katibu lakini cha kushangaza vikao vinapoitishwa kumekuwapo   mgongano mkubwa kati ya mwenyekiti na katibu.

“Katibu akiitisha kikao,   mwenyekiti naye anaitisha kikao,   sasa sisi wajumbe tunashindwa kuhudhuria vikao hivyo maana wanakuwa wanatuchanganya.

“Nimefika leo mbele ya waandishi wa habari na nasema   nimejitoa kwenye uanachama na kurudisha kadi kwa sababu ya mgongano wa  maslahi kwa mwenyekiti na katibu.

“Baada ya kutoka   ACT Wazalendo nimeamua kurudi kwenye changu cha zamani Chama Cha Mapinduzi (CCM),” alisema Lolottu.

Naye Katibu wa Jimbo la ACT Wazalendo Babati Vijijini na Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana  Mkoa wa Manyara, Maurine Plasidi alisema yeye hawezi kwenda kwenye sera moja na watu ambao hawaeleweki.

Katibu wa   ACT Mkoa wa Manyara, Francis Matle alisema umekuwapo mwingiliano wa  madaraka wa viongozi wa ngazi mbalimbali yakiwamo majimbo.

Alisema hiyo ni  baada ya uongozi wa mkoa kutofautian  jambo ambalo ofisi ya katibu mkuu  inalijua.

“Nimefikia uamuzi huu na nataka wananchi na watanzania wote kwa ujumla wajue kwamba mgogoro huu umekuwa mkubwa na unaendelea kuharibu taswira ya chama.

“Nmeamua kuachia ngazi na kujitoa uanachama na kurududisha kadi, nyaraka zote nazipeleka ofisi ya CCM kwenda kuzihifadhi huko kwa sababu  huko ndiko kwenye usalama zaidi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles