Na BEATRICE MOSSES, Babati
VIONGOZI watatu wa Chama cha Alliance for Change and Transpancy (ACT) Wazalendo Mkoa wa Manyara wamejiuzulu nafasi zao.
Vilevile wamejitoa uwanachama wakidai uelekeo wa chama hicho si mzuri.
Walisema wamefikia uwamuzi huo baada ya kuona mwenyekiti na katibu wa chama hawaelewani.
Katibu wa Ngome ya Wazee ACT Mkoa wa Manyara, James Lolottu, alisema a hivi karibuni kulikuwa na mgogoro kati ya katibu wa mkoa wa chama hicho na mwenyekit wake.
“Tumepata matatizo hapa katikati, kama katiba ya ACT Wazalendo inavoeleza.
“Anayehusika kuitisha vikao vya chama ngazi ya mkoa ni katibu lakini cha kushangaza vikao vinapoitishwa kumekuwapo mgongano mkubwa kati ya mwenyekiti na katibu.
“Katibu akiitisha kikao, mwenyekiti naye anaitisha kikao, sasa sisi wajumbe tunashindwa kuhudhuria vikao hivyo maana wanakuwa wanatuchanganya.
“Nimefika leo mbele ya waandishi wa habari na nasema nimejitoa kwenye uanachama na kurudisha kadi kwa sababu ya mgongano wa maslahi kwa mwenyekiti na katibu.
“Baada ya kutoka ACT Wazalendo nimeamua kurudi kwenye changu cha zamani Chama Cha Mapinduzi (CCM),” alisema Lolottu.
Naye Katibu wa Jimbo la ACT Wazalendo Babati Vijijini na Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Mkoa wa Manyara, Maurine Plasidi alisema yeye hawezi kwenda kwenye sera moja na watu ambao hawaeleweki.
Katibu wa ACT Mkoa wa Manyara, Francis Matle alisema umekuwapo mwingiliano wa madaraka wa viongozi wa ngazi mbalimbali yakiwamo majimbo.
Alisema hiyo ni baada ya uongozi wa mkoa kutofautian jambo ambalo ofisi ya katibu mkuu inalijua.
“Nimefikia uamuzi huu na nataka wananchi na watanzania wote kwa ujumla wajue kwamba mgogoro huu umekuwa mkubwa na unaendelea kuharibu taswira ya chama.
“Nmeamua kuachia ngazi na kujitoa uanachama na kurududisha kadi, nyaraka zote nazipeleka ofisi ya CCM kwenda kuzihifadhi huko kwa sababu huko ndiko kwenye usalama zaidi,” alisema.