22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

VICTOR MOSES: WAZAZI HAWAYAJUI MAFANIKIO YANGU

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO


Victor Moses
Victor Moses

KATIKA wachezaji ambao wanaaminika kwa kiasi kikubwa na kocha wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, ni mshambuliaji wa pembeni wa klabu hiyo, Victor Moses, ambaye ameonekana kuonyesha kiwango kizuri msimu huu.

Awali mchezaji hiyo alikuwa anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, lakini kutokana na uwezo wake kuwa mkubwa kocha wa klabu hiyo alijaribu kumchezesha nafasi ya mshambuliaji wa pembani kwa upande wa kulia.

Tangu Oktoba mwaka huu, mchezaji huyo ameonekana kuitumikia vizuri nafasi hiyo hivyo kujihakikishia namba ya kudumu katika kikosi hicho cha Conte.

Moses ni raia wa nchini Nigeria ambaye anadai kuwa anajisikia vibaya kuwa na mafanikio makubwa kwa sasa bila ya wazazi wake kuona na kufaidi mafanikio hayo ya mtoto wao.

Mchezaji huyo alipoteza wazazi wake huku akiwa na umri wa miaka 11, wakati huo kwa sasa ana umri wa miaka 25, wazazi hao walifariki siku moja nchini Nigeria katika mapigano ya dini.

Baba wa Moses alikuwa anajulikana kwa jina la Mr Austine huku mama akijulikana kwa jina la Mrs Josephine Moses, ambapo Mr Austine alikuwa na mchungaji hivyo familia hiyo ilikuwa ni watu wa dini, lakini mwaka 2002 kulikuwa na mgogoro wa kidini kati ya Wamishenari na Waislam ambapo mapigani hayo yalifika hadi kwenye nyumba yakina Moses na kuwavamia wazazi wake kisha kuwaua.

Wakati wazazi hao wanauawa, Moses alikuwa mtaani anacheza mpira na vijana wenzake na baadae akapata taarifa kwamba nyumbani kuna uvamini wa watu wa dini, alipokwenda akakuta wazazi wake tayari wameuawa.

Kitendo hicho kilimpa wakati mgumu kwa kuwa tayari alipata vitisho kwamba wauaji hao baadae watakuja kwake kwa ajili ya kumuua hivyo wale rafiki zake ambao alikuwa anacheza nao mpira waliamua kushirikiana kwa ajili ya kumficha kwa kuwa walikuwa wanampenda kutokana na uwezo wake wa kucheza soka.

Baada ya muda mjomba wake kutoka jijini London, alimfanyia mpango wa kumsafirisha kwa ajili ya kuishi naye pamoja, hivyo Moses alikimbilia London nchini Uingereza kwa mjomba wake huku akiwa na miaka 11.

Baada ya kufika huku alimpeleka shule ambapo alionesha uwezo wa kucheza soka kama alivyofanya nchini Nigeria, bado akiwa na umri mdogo alipata nafasi ya kuitumikia timu ya vijana wadogo ya Crystal Palace, lakini ilipofika mwaka 2007 alipata nafasi ya kucheza timu ya wakubwa hadi mwaka 2010.

Baadae alijiunga na timu ya Wigan hadi 2012, ambapo alianza kuyaona mafanikio makubwa, hata hivyo wakati huo alipata nafasi ya kucheza timu ya taifa ya Uingereza kwa vijana chini ya umri wa miaka 16,17,19, na 21.

Wakati anazitumikia timu hizo za vijana nchini England bado alikuwa na moyo wa kutaka kurudi nchini Nigeria kwa ajili ya kulitumikia taifa lake japokuwa kuna wabaya wake ambao waliwateketeza wazazi wake.

Bado alikuwa na moyo wa utaifa, hivyo mwaka 2012 alipata nafasi ya kujiunga na klabu ya Chelsea hapo ndipo alifanya maamuzi ya kurudi nchini Nigeria kwa kuitumikia timu ya taifa. Alidai kuwa mara ya kwanza anakuja Nigeria kwa ajili ya kuitumikia timu ya taifa alikuwa na furaha kubwa kwa kuwa aliona mashabiki wengi wakiwa wamevaa jezi za Chelsea na kushangilia kwa kulitaja jina lake.

“Nilikuwa na furaha kubwa kuona mashabiki wengi wakiwa wanalitaja jina langu huku wakiwa wamevaa jezi za Chelsea, niliamini kuwa Afrika mashabiki wengi wanapenda soka, hivyo nilifurahi kuliwakilisha taifa langu.

“Niliamua kujitolea kwa ajili ya taifa, nina ndugu wengi Nigeria, marafiki na mashabiki, hivyo niliona bora nifanye maamuzi hayo, lakini nilikuwa na uchungu kwamba wazazi wangu hawapo na kama wengekuepo basi wangeona jinsi gani ninavyo pigania taifa langu.

“Leo hii natapa wakati mgumu nikipigania maisha yangu kuwa na mafanikio makubwa katika ulimwengu wa soka lakini wazazi wangu hawapo, ni jambo ambalo limekuwa likiniumiza kwa kiasi kikubwa sana.

“Lakini bado ninaamini mafanikio haya yanatokana na dua za wazazi wangu kwa jinsi walivyoniacha, hivyo ninajivunia kuwa hapa kwa sasa na bado nina ndoto za kufanya makubwa katika soka na ikiwezekana siku moja nije kuitumikia klabu ya Barcelona,” alisema Moses.

Leo hii kile kizazi ambacho kilikuwa na mgogoro na familia ya Moses ni wazi wanakuwa na furaha mchezaji huyo akiwa anaitumikia timu ya taifa na kufanya vizuri katika michuano mikubwa ya kimataifa.

Hata hivyo, mchezaji huyo amedai kuwa lengo lake kubwa ni kuhakikisha taifa hilo linafanikiwa kutwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika, pia amedai kuwa hana mpango wa kufikiria kilichotokea miaka hiyo iliyopita na kama wapo ambao walifanya hivyo kwa upande wake amewasamehe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles