24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Viatu vya Jordan vyauzwa bil. 3/-

LOS ANGELES, Marekani

JOZI moja ya viatu alivyokuwa akitumia staa wa Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA), Michael Jordan, vimeuzwa kwa Dola za Marekani milioni 1.47 (zaidi ya Sh bil. 3 za Tanzania).

Jordan ambaye ameshastaafu, alitumia viatu hivyo vyeupe vya Nike mwaka 1984, wakati huo ukiwa ni msimu wake wa kwanza NBA akiwa na Chicago Bulls.

Bei hiyo ya Dola milioni 1.47 iliyopatikana kwenye mnada, ni kubwa zaidi kuwahi kutokea kwa viatu vya mchezo wowote duniani.

Kwa wasiofahamu, Jordan aliyeachana na kikapu mwaka 2003, ndiye mchezaji wa kwanza wa NBA kuwa bilionea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles