*Lengo ni kutoa ajira kwa vijana
Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital
Katika kukabiliana na wimbi la ajira nchini VETA Shinyanga na Dodoma inaendesha mafunzo ya ususi na urembo ili kuwapatia ajira vijana.
Akizungumza leo Juni 30, jijini Dar es Salaam, Mwalimu wa Ususi na Urembo VETA Dodoma, Hamisa Amir amesema wanatoa mafunzo ya ususi na urembo kuanzia umri wa miaka 18-35 kwa vijana ambao hawajui kabisa na wenye ujuzi miaka 18 na kuendelea.
Amesema sekta ya urembo inakua kwa kasi kwa sababu wanaosoma fani hiyo wameongezeka ikiwa tofauti na miaka ya nyuma na wanaangalia mitindo inayoendana na soko la duniani.
“Mafunzo hayo tunatoa shinyanga, Dodoma, Iringa, Dar es Salaam na mikoa mingine tuna malengo makubwa na kuhakikisha vijana wanapata ajira kupitia sekta hii na tunatoa mafunzo ya wiki moja,” amesema Hamisa.
Amesema vijana kupata elimu ya matumizi ya vifaa kuepusha madhara kwa wateja na ambao hawaruhusiwi ikiwemo wajawazito na watu wenye presha.
Hamisa amesema asilimia 99 ya vijana wengi fani hii wanajifunza mtaani hivyo ni vigumu kupata ajira.
Aidha amesema changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni vijana wengi kutokuwa na elimu ya Ususi na urembo wanao hudumia wengi hawana taaluma.
“Vijana wa kiume wanasoma fani hii ni wachache wanakuwepo wawili hadi watano wengi wanajifunza mtaani ambao hawana ujuzi inapelekea kuharibu nywele za wateja hawana huduma kwa mteja,”amesema.