Vanessa awataka wasanii kutumia falsafa ya ‘hapa kazi tu’

0
655

Vanessa-mdeeNA MWANDISHI WETU

 MSANII Vanessa Mdee ambaye ni mmoja wa wanamuziki wanaoshiriki onyesho la Coke Studio linaloendelea, amewaasa wanamuziki wa Tanzania kufanya kazi kwa bidi na kuzingatia falsafa ya ‘hapa kazi tu’ iliyoanzishwa na Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, John Magufuli.

Akizungumza na vijana juu ya mafanikio yake jijini Dar es Salaam jana, Vanessa alisema kuwa mafanikio aliyonayo hayakuja kama mvua, bali yametokana na kufanya kazi kwa bidii, kujiamini na kuwa mbunifu.

“Mafanikio yoyote yanataka kujituma, hivyo ni muhimu kwa wasanii wachanga na wakongwe kufanya kazi kwa bidii zaidi ili wapate mafanikio na nawahakikishia kuwa kazi ya muziki inalipa na inaweza kutoa ajira kwa vijana wengi,” alisema Vanessa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here