Goodluck kuachia albamu yake leo

0
779

goodNA CHRISTOPHER MSEKENA

NYOTA wa muziki wa Injili nchini, Goodluck Gozbert, leo anatarajia kukata kiu ya mashabiki wake kwa kuachia albamu ya kwanza inayoitwa ‘Ipo Siku’, mara baada ya kimya kirefu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Goodluck alisema sababu zilizo nje ya uwezo wake zilifanya aicheleweshe albamu hiyo, lakini anatarajia atawafurahisha mashabiki wake kwa kutoa albamu yenye nyimbo zilizobeba ujumbe mzito kwa watu wote.

“Ni albamu nzuri kuisikiliza, ina nyimbo za kutia moyo kwa waliokata tamaa, ukisikiliza nyimbo zangu zilizotangulia kama Acha Waambiane na Ipo Siku utabaini ni jinsi gani albamu hii ilivyo na nyimbo nzuri, kwa sasa inapatikana madukani kote watu wanaweza kujipatia nakala zao,” alisema.

Aliongeza kuwa albamu hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo nane ambazo ni Nimesamehe, Pendo Langu, Ndiwe Mungu, Moyo Tulia, Surprise, Acha Waambiane na Ipo Siku iliyobeba jina la albamu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here