27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Kardashian: Nimepoteza kilo 7 baada ya kujifungua

kimCHICAGO, MAREKANI

NI siku 10 tangu Kim Kardashian apate mtoto wa pili, lakini mrembo huyo amesema kwa sasa amepungua uzito wa kilo 7 tangu alipojifungua.

Mrembo huyo wakati ana ujauzito wa mtoto wake, Saint alikuwa na uzito wa kilo 86, lakini baada ya kujifungua amejikuta akipoteza kilo 7 na anadai bado ataendelea kupunguza ili awe kama wakati anaolewa na mume wake, Kanye West.

“Wakati ninaolewa na Kanye West nilikuwa na uzito wa kilo 53, lakini nilipopata ujauzito wa Saint kilo zilizidi kuongezeka, kwa sasa nimeanza kupoteza uzito kwa kiasi kikubwa kwa muda mfupi na ninaamini nitaendelea kupunguza na kuwa kama awali.

“Wakati nilipokuwa na ujauzito nilijiona kama naelekea kufa kwa kuwa nilikuwa na uzito mkubwa sana, ila nitaanza kufanya mazoezi kwa ajili ya kuziweka sawa kilo zangu,” alisema Kim.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles