Vanessa awashukuru mashabiki wa Instagram

0
1056

vanessaMdee_001_lrgNA MWANDISHI WETU

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Vanessa Mdee, amewashukuru mashabiki wa mtandao wa Instagram kwa kumuunga mkono na kufanya afikishe wafuasi milioni moja.

Venessa anaungana na wakali kama Diamond Platnumz, Millard Ayo, Jokate Mwegelo, Jackline Wolper na Wema Sepetu ambao ni watu maarufu wachache wenye wafuasi wengi kwenye mtandao huo.

Akiwashukuru mashabiki wake, Vanessa alisema moja ya mtaji mkubwa kwenye biashara ya muziki ni watu hivyo idadi hiyo kubwa ya wafuasi inaonyesha ni jinsi gani biashara yake inakua.

“Mashabiki ni mtaji, wasanii tunafanya kazi kwa ajili ya watu ndiyo maana nimefurahi kufikisha idadi hii ya mshabiki milioni moja kwenye Instagram, ni ishara nzuri kuwa kazi zangu zinakubalika,” alisema Vanessa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here