26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Wakorintho wapili kuzindua Mchepuko sio dili

Alex+MsamaNa Mwandishi Wetu

KWAYA ya Wakorintho Wapili ya Wilayani Mafinga, mkoani Iringa, inatarajia kuzindua albamu yake ya Mchepuko sio dili kwenye tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, amesema albamu hiyo ya Mchepuko sio dili ina nyimbo nane ambazo zinafikisha ujumbe  wa neno la Mungu kwa jamii.

Msama alizitaja nyimbo hizo ni pamoja na Tanzania, Mchepuko sio dili, Watenda mabaya, Ee bwana, Yahwe tunakuinua, Tuokoe baba, Dunia hii na Hana.

Aidha Msama alisema maandalizi ya kuelekea katika tamasha hilo yanaendelea vizuri, hivyo Watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kuelekea tamasha hilo.

Aliongeza kuwa watanzania walichukilie tamasha hilo kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kutupitisha katika kipindi kigumu cha uchaguzi Mkuu ambao ulifanyika kwa amani na utulivu ingawa kulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani.

Msama alisema waimbaji wa Tanzania watakaosindikiza tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkobe, Joshua Mlelwa, Martha Mwaipaja, Jesca BM,  na Christopher Mwahangila, Sifael Mwabuka sambamba na Kwaya ya Yombo KKKT.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles