27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Van Gaalawapamtihani United

Manchester_UnMANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Manchester United, Louis van Gaal, amewapa changamoto wachezaji wake kuthibitisha kuwa wao ni washindani halisi kwenye kupigania taji la Ligi Kuu England kwa kuwafunga watani zao wa jadi,Manchester City Jumapili hii.

United imerejea kwenye mwendo wake wa ushindi baada ya juzi kuichapa Everton mabao 3-0, huku vinara Man City wakiiua Bournemouth 5-1 katikaUwanja w aEtihad.

Mabao ya United yaliyofungwa na Morgan Schneiderlin, Ander Herrera na Wayne Rooney, ambaye alifunga bao la pili dhidi ya timu yake hiyo ya zamani kwenye Uwanja wa Goodison Park.

“Daima huwa tuna malengo ya kuwa mabingwa. Hiyo bila shaka ni muhimu katika tamaa yetu,” alisema Van Gaal.

United inatakiwa kuifunga Man City kwenye mchezo ujao utakaofanyika Uwanja wa Old Trafford, ili kuondoa pengo la pointi mbili na kukaa kileleni.

“Nina furaha sana na namna wachezaji wangu walivyonijibu baada ya kuhitaji ushindi na nimefarijika na kucheza kwao vizuri,” alisema Mholanzi huyo.

“Nafikiri tulikuwa na kiwango kizuri sana na nadhani huu ni mwanzo wa ushindi mwingi tunapoelekea. Tunatakiwa kuendelea hivi wiki ijayo (wiki hii) tutakapocheza na Manchester City, halafu ndipo tutakaposema labda tupo sawa kuchukua ubingwa.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles