24.1 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

Neymar, Sterling, Kruse watikisa kwa ‘hat trick’

neymar-jrCATALOUNIA, HISPANIA

NYOTA wa timu ya Barcelona, Neymar Jr, juzi aliifungia mabao manne timu yake wakati ikiilaza Rayo Vallecano
mabao 5-2 na kulingana pointi na vinara wa Ligi Kuu Hispania, Real Madrid.

Wakati Neymar akifunga ‘hat trick’ ya kwanza msimu huu, akilingana na mchezaji mwingine wa Ligi Kuu England, Raheem Sterling, aliyefunga mabao matatu Manchester City ikishinda mabao 5-1.

Pia kwenye Ligi Kuu Ujerumani (Bundersliga), mshambuliaji wa Wolfsburg Max Kruse, naye alifunga ‘hat trick’ wakati timu yake ikiilaza TSG Hoffenheim 4-2.

Barca ikitoka nyuma kwa bao walilotanguliwa kufungwa mapema na Javi Guerra, imeshinda kwa mara ya pili kwenye mechi nne zilizopita za ligi.

Neymar amefanya makubwa hayo wakati Lionel Messi akikosekana kwa majeruhi yanayomkabili, amekuwa Mbrazil wa kwanza kufunga mabao manne kwenye La Liga tangu Julio Baptista, alipofanya hivyo mwaka 2004 alipokuwa Sevilla.

Staa huyo, 23, amefikisha jumla ya mabao nane msimu huu yaliyomfanya kuwa kileleni kwenye ufungaji bora, ambapo kwa mujibu wa takwimu Barcelona imeruhusu mabao 11 katika mechi nane za La Liga, msimu
uliopita hadi kufikia sasa walikuwa hawajaruhusu bao lolote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles