25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Jose Mourinhoamkomalia Eden Hazard

Manchester United v Chelsea - Premier LeagueLONDON, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Chelsea, Jose Mourinho, amemwambia winga wake,Eden Hazard, ataendelea kuanzia benchi mpaka pale atakapofanya majukumu ya ukabaji kama vile Willian na Pedro.

Mchezaji huyo bora wa kulipwa England (PFA) msimu uliopita, juzi alianzia benchi wakati timu hiyo ilipoichapa Aston Villa mabao 2-0, ukiwa ni ushindi wao wa tatu msimu huu.

Mourinho baada ya mchezo huo amesema Hazard anatakiwa kufanya kazi ya ziada kushinda mtihani wa kurudisha nafasi yake.

“Nimemuweka nje Hazard kwa sababu tuliruhusu mabao mengi. Tunatakiwa kuzuia vema…Kama hatuna mpira, ubora hauna chochote na hapo inamaanisha…kama unao au hauna,” alisema Mourinho.

“Ni uamuzi wa kiufundi zaidi kumuacha benchi mchezaji bora, lakini yote ni kuleta nidhamu ya kimbinu na naamini timu itaweza kuwa imara.

“Willian na Pedro walifanya kazi kubwa nzuri ya kuzuia na kuwafanya viungo kuwa vizuri zaidi. Nitaendelea na njia hiyo au yeye kuingia na kufanya kazi ileile wanayofanya Willian na Pedro.”

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles