29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Van Gaal apewa michezo miwili kulinda kibarua chake

van-gaalMANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal, amepewa michezo miwili ya kufanya vizuri ili kuweza kulinda ajira yake ndani ya timu hiyo.

Baada ya Manchester United kupokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Norwich kwenye uwanja wa nyumbani katika michuano ya Ligi Kuu, bodi ya klabu hiyo ilikaa na kuchunguza maendeleo ya klabu hiyo ambapo wamepanga kumpa michezo miwili.

Endapo kocha huyo atashindwa kufanya vizuri katika michezo huyo, basi ataungana na Jose Mourinho, ambaye amefukuzwa wiki iliyopita katika klabu yake ya Chelsea.

Michezo ambayo anaisubiri Van Gaal ni dhidi ya Stoke City siku ya ‘Boxing Day’, kwenye Uwanja wa Britannia na mchezo dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa nyumbani wa Old Trafford Desemba 28.

Hii ni michezo ambayo inaonekana kumpa wakati mgumu kocha huyo ili kuweza kujipa matumaini ya kuendelea kuwa kocha wa klabu hiyo.

Lengo kubwa la uongozi wa klabu hiyo ni kuona timu yao ikibadilika na kupigania ubingwa wa michuano ya Ligi Kuu, huku ikiwa tayari imetolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Klabu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi nchini England, huku ikiwa na alama 29, lakini Van Gaal anaamini kuwa anaweza kufanya vizuri kama atashirikiana vizuri na wachezaji wake.

“Kwa sasa tupo katika wakati mgumu, tumepoteza michezo miwili, hivyo inawafanya mashabiki kuwa na wasiwasi, lakini kama wachezaji wataonesha ushirikiano basi tutafanikiwa kufanya vizuri,” alisema Van Gaal.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles