29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Blatter, Platini kifungoni miaka nane

Sepp Blatter, left, and Michel Platini shortly after the former had been re-elected Fifa presidentZURICH, USWISI

RAIS wa Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA), Sepp Blatter na Rais wa Vyama vya Soka barani Ulaya (UEFA), Michel Platini, wamefungiwa kujishirikisha katika soka kwa miaka nane.

Maamuzi hayo yametokea baada ya uchunguzi uliofanyika na kugundulika kwamba viongozi hao walijihusisha na rushwa ya pauni milioni 1.35 Februari 2011.

Kamati ya maadili ya shirikisho hilo ikiwa chini ya Mwenyekiti wake, Hans Joachim Eckert, imethibitisha kwamba Blatter na Platini wamefungiwa kushiriki katika soka kwa miaka nane.

Kutokana na matukio mbalimbali ya viongozi hao, Blatter alitakiwa kulipa faini ya pauni 33,700, wakati Platini akitakiwa kulipa faini ya pauni 53,940.

Tuhuma za rushwa zilianza kuwa wazi mara baada ya Blatter kuteuliwa kwa mara ya tano ya nafasi ya urais katika shirikisho hilo Mei, mwaka huu ikiwa ni siku nne tangu ateuliwe.

Blatter aliamua kutangaza kujiuzulu wadhifa wake ambapo uchaguzi mkuu ukapangwa ufanyike Februari 26, mwakani, wakati huo Platini akitangaza kuwania nafasi hiyo.

Kutokana na hali hiyo, ni wazi kwamba Platini ambaye alionekana kuwa na idadi kubwa ya mashabiki ambao walimpa nafasi ya kuwa rais mpya wa Fifa hapo mwakani, mipango yake itagonga mwamba kutokana na kifungo hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles