25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Lampard avunja ukimya, afunga ndoa na Christine

LampardLONDON, ENGLAND

NYOTA wa zamani wa klabu ya Manchester City na Chelsea, Frank Lampard, amefanikiwa kufunga ndoa juzi na mke wake ambaye ni mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha BBC nchini England, Christine Bleakley.

Kiungo huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya England mwenye umri wa miaka 37, ameamua kukamilisha ahadi yake baada ya kukaa kwenye uchumba kwa miaka minne na Christine.

Ndoa hiyo ilifungwa kwenye Kanisa la St Paul’s lililopo Knightsbridge, jijini London, ambapo wachezaji mbalimbali walijitokeza katika sherehe hiyo.

Kocha wa zamani wa mchezaji huyo, Jose Mourinho, ambaye amefukuzwa kazi katika klabu ya Chelsea, alionekana kuwa wa kwanza kufika katika eneo hilo ambalo Lampard alifungia ndoa yake.

Katika sherehe hizo nyota wa Manchester United, Wayne Rooney na Rio Ferdinand, walikuwa katika orodha ya wageni waalikwa, huku wakiwa sambamba na wachezaji wengine kama vile John Terry, Branislav Ivanovic na Petr Cech.

Lampard kwa sasa anakipiga katika klabu ya New York City ya nchini Marekani, baada ya kuondoka Manchester City ambapo alidai kwamba anataka kwenda kumaliza soka lake huko Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles