22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Andy Murray atwaa tuzo ya tenisi ya BBC

Andy MurrayBELFAST,IRELAND

NYOTA wa mchezo wa tenisi, Andy Murray, ameibuka kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa tenisi wa BBC baada ya kuwazidi wapinzani wake kwa kura nyingi.

Tuzo hizo ambazo zilifanyika huko Ireland ya Kaskazini, Murray alifanikiwa kushinda kwa idadi ya kura 361,446, sawa na asilimia 35 dhidi ya Kelvin Sinfield ambaye alipata kura 278,353, sawa na asilimia 28 na Ennis Hill akipata kura 78,898, sawa na asilimia 8.

Hii ni mara ya pili kwa Murry kuchukua tuzo hiyo, na mwaka huu ameonekana kuboresha kiwango chake na amefanikiwa kufikia fainali za mashindano ya Australia na fainali za Wimbledon.

“Nashukuru sana kufanikiwa kuchukua tuzo hii kwa kuwa sikutegemea, lakini leo nina furaha kubwa na ninaamini kila kitu kinawezekana katika maisha.

“Hii ni safari ya miaka mitano kwenye tenisi, nilianza kama utani nikishika nafasi ya mwisho, lakini leo hii najikuta nikishika nafasi ya kwanza, nashukuru sana,” alisema Murray.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles