26 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Uwanja wa Azam kufungwa

Theresia Gasper -Dar es salaam

UONGOZI wa klabu ya Azam FC, umesema unatarajia kufunga uwanja wao kwa ajili ya kuufanyia marekebisho yatakayochukua muda wa mwezi mmoja na nusu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jafar Idd, alisema kuanzia Desemba 3 mwaka huu, uwanja huo utafungwa na kuanza kwa marekebisho hayo.

“Tunahitaji kuwa na uwanja bora, hivyo mafundi wetu wametuambia ukarabati huu utachukua mwezi mmoja na nusu, ambapo utaanza kutumika tena mara baada ya kutoka michuano ya Kombe la Mapinduzi,” alisema.

Alisema mbali na uwanja pia watafanya marekebisho katika sehemu nyingine ambazo zitahitajika ili wawe bora zaidi.

Akizungumzia timu yao Idd alisema mara baada ya kumaliza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Alliance, wachezaji wao walirejea na kuendelea na programu nyingine.

Azam katika mchezo wao wa mwisho waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Alliance katika Uwanja wa Nyamagana Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles