24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

‘Alikiba Unforgettable Tour’ kuacha historia Tabora

Mwandishi Wetu -Tabora

HERI ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa  Mfalme wa Bongo Fleva, Alikiba ambaye jana alitimiza miaka kadhaa na kuwa neema kwa maelfu ya wakazi wa Tabora, sehemu aliyochagua kuzindua ziara yake ya Alikiba Unforgettable Tour.

Kiba ambaye alitua mkoani humo, Jumatano wiki hii alipokewa kifalme kutoka Uwanja wa Ndege mpaka kwenye mitaa mbalimbali ya mji huo huku mamia ya mashabiki waliokuwa wanatumia usafiri wa pikipiki, magari na miguu wakimpigia shangwe.

Baada ya kushangazwa na mapokezi mazuri aliyoyakuta kwenye mji huo maarufu kama Toronto, Kiba alisema “Saluti sana Tabora, nimefurahi kwa mapokezi yenu makubwa, naomba siku ya tarehe 30 (leo ) tunaingia uwanjani kufanya shoo.”

Kama alivyokuwa ametangaza hapo awali kuwa kwenye ziara hiyo ya kuwashukuru mashabiki waliompa sapoti kwa miaka 17 ya uwepo wake kwenye muziki, Kiba alitangaza ‘Medical Camp’ kwaajili ya kupima afya na kutoa dawa bure kwa wakazi wa mji huo.

Lakini hali ya hewa na masual ya usalama, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ikashauri vitu vilivyoandaliwa kaawajili ya ‘Medical Camp’ vipelekwe hospitali ya Mkoa sababu vitawanufaisha wakazi wa mkoa huo.

Hatimaye juzi, Kiba akiongozana na Mkuu wa Mkoa, Aggrey Mwanri alifika katika hospitali ya Kitete kutoa misaada hiyo inayokadiliwa kuwa na thamani ya shilingi 6,000,000 ili wakazi wa mji huo wanufaike na ziara hiyo.

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa tiba, Mkuu wa Mkoa  alimpongeza Alikiba kwa mchango wake kwenye jamii huku akikisitiza watu wa Tabora kuthamini afya zao.

“Tujenge tabia ya kucheki afya zetu hapa, watu hawali papai au mchicha mpaka waandikiwe na Daktari, wanatutumuka na chips, AliKiba anakuja hapa kusapoti ili Tabora iwe kama Toronto, tunakuombea Kiba pia tunaombea tupate akina Alikiba wengi,” alisema Mwanri.

Mbali na masuala ya afya, Alikiba Unforgettable Tour jana iliacha historia katika Mkoa huo baada ya Alikiba kuzungumza na kuwajengea ndoto kazi vijana wanaosoma Chuo cha Ardhi, Tabora.

Baada ya kuzungumza na vijana, Kiba na timu yake waliingia kwenye Uwanja wa Chipukizi na kucheza mechi ya kirafiki na timu ya wakazi wa Tabora.

Katika kuzindua ziara yake ambayo itapita kwenye miji mbalimbali Tanzania, leo jioni Kiba, Kings Music na wasanii marafiki wanatarajiwa kudondosha burudani ya kukata na shoka katika viwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Onyesho hilo litakaloambana na sherehe ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake, Kiba ametamba kuwa itakuwa bab kubwa kwani toka aanze muziki hakuwahi kufika Tabora hivyo ana kiu ya kutoa burudani na kuacha historia itakayomtambulisha kama Mfalme wa Bongo Fleva.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles