23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM YAKUNWA UTENDAJI WA DK. SHEIN


Na MWANDISHI WETU-ZANZIBAR

UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM), umesema unaridhishwa na utendaji wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar chini ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein.

Hayo yalisemwa Ikulu mjini Unguja juzi na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James, alipokutana na Dk. Shein.

Katika kikao hicho Kheri aliambatana na Makamu Mwenyekiti UVCCM, Tabia Maulid Mwita, Kaimu Katibu Mkuu, Shaka Hamdu Shaka na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Abdulghafar Idrissa Juma.

Akizungumza katika kikao hicho, Kheri alisema uongozi wa UVCCM, unafurahishwa namna ambavyo Dk. Shein anavyoendelea kujali, kuthamini na kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wananchi kwa wakati.

“Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais Dk Ali Mohamed Shein, imeendelea kujali, kuthamini na kushughulikia shida, kero na matatizo ya wananchi hatimaye kuyapatia ufumbuzi stahili. UVCCM tumeridhishwa mno na kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/20,” alisema.

Kheri, alitumia nafasi hiyo kuwaasa vijana kuwa na desturi ya kwenda kuchota busara na hekima toka kwa wazee kama njia ya kukomaa kisiasa.

“Vijana mnapokwenda kwa wazee, kiuhalisia mnakwenda kuchota busara na hekima. Vijana bila ya msukumo wa fikra na mawazo ya wazee, hatuwezi kujifunza jambo lolote na kukomaa kisiasa. UVCCM tumeridhika na utendaji wa SMZ katika mkakati wa kuzitazama shida na maisha ya wananchi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles