30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

JPM: OLE WAO

MARUFUKU MICHANGO: Rais Dk. John Magufuli akizungumza bada ya kukutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo (kushoto) na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako Ikulu jijini Dar es salaam jana ambapo amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza mawaziri hao kusimamia hilo.
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli, ameagiza kuchukuliwa hatua dhidi ya viongozi na watendaji ambao shule za msingi na sekondari zilizopo katika maeneo yao zinawatoza wanafunzi michango mbalimbali kinyume na mwongozo wa Serikali wa utoaji elimu bila malipo.

Agizo hilo amelitoa Ikulu Dar es Salaam jana, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo.

Alisema Serikali inatoa Sh bilioni 23.875 kila mwezi kuwezesha utoaji elimu bila malipo, lakini alishangazwa kuona bado kuna walimu wanaendelea kuwatoza michango ama kuwarudisha nyumbani wanafunzi ambao wanashindwa kutoa.

“Nawaagiza mawaziri, sitaki kusikia mwanafunzi anarudishwa nyumbani kwa kushindwa kutoa michango, na fikisheni maagizo haya kwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi, na wote wanaohusika. Nikisikia tena mahali jambo hili linaendelea, hawa niliowateua mimi wataondoka.

“Haiwezekani tumefuta ada, halafu walimu wanaamua kuanzisha michango, tena mikubwa ambayo watu masikini wanashindwa kusomesha watoto wao, na kama wazazi wanataka kuchangia kitu shuleni, wapeleke michango yao kwa mkurugenzi, lakini sitaki kusikia mwanafunzi anapewa sharti la kutoa mchango ndipo apokelewe shule,” alisema.

Rais Magufuli alitoa maagizo hayo baada ya kupata taarifa kuwa zipo baadhi ya ……………………….

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles