27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

KAMATI YA TANZANITE, MGODI WAANZA MAZUNGUMZO


Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KAMATI iliyoundwa na Rais Dk. John Magufuli kuchunguza biashara ya madini ya Tanzanite, imeanza kufanya mazungumzo na Kampuni ya Tanzanite One.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.

Alisema mazungumzo hayo yaliyoanza Januari 16, mwaka huu, yanalenga kuhakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo na rasilimali ya madini hayo ambayo yanachimbwa Tanzania pekee.

Profesa Kabudi alisema mazungumzo hayo yameanza vizuri na pande hizo mbili zinapitia matatizo yote yanayohusu biashara ya madini ya Tanzanite, utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali za madini na mapato ya rasilimali hiyo, ili hatimaye zikubaliane namna bora itakayohakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tanzanite One, Faisal Shahbhai, alisema kampuni hiyo ipo tayari kwa majadiliano hayo na inaunga mkono juhudi za kuhakikisha madini hayo yanainufaisha Tanzania tofauti na ilivyo sasa yanazinufaisha zaidi nchi nyingine ambazo haziyazalishi.

Alisema kuwa Tanzanite One itatoa taarifa zote zinazohitajika na wakati wote itatoa ushirikiano wenye lengo la kufanikisha mazungumzo hayo.

Novemba 17, mwaka jana, Spika wa Bunge, Job Ndugai, aliunda kamati mbili zitakazoshughulikia sekta ya uvuvi wa bahari kuu na gesi, akisema lazima wajue ni kwanini hazichangii pato la taifa.

Ndugai ameunda kamati hizo baada ya nyingine mbili za kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na almasi kuwasilisha taarifa kwa Rais Magufuli Septemba, 2017 na kusababisha baadhi ya mawaziri kujiuzulu.

Ndugai akitangaza kamati hizo, alisema anatumia kanuni ya 5(1) ya kanuni za Bunge toleo la 2016 ambayo inampa madaraka ya kuziunda kwa kadiri atakavyoona inafaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles