25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

LAAC YATILIA SHAKA GHARAMA ZA UJENZI WA SHULE

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imetilia mashaka mradi wa vyumba viwili vya madarasa wa Shule ya Sekondari ya Ndaoya iliyopo jijini Tanga.

Akizungumza shuleni hapo Mjumbe wa kamati hiyo, Joseph Selasini amesema mabati yaliyotumika kuezeka vyumba hivyo hayalingani na gharama elekezi za mradi huo jambo lililowakera wabunge hao.

Amesema ni vema kila halmashauri nchini ikatekeleza miradi yote kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni ili kulinda fedha za serikali.

Katika hatua nyingine Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Abdallah Chikota ameushauri uongozi wa halmashauri ya jiji la Tanga kupitia upya mikataba ya uwekezaji upande wa ardhi ili kuepuka hasara ya maeneo mengi kutelekezwa na baadhi ya wawekezaji, kama ilivyo katika maeneo mbalimbali nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles