27.6 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

UVCCM YACHAMBUA UTENDAJI WA DK. SHEIN

Na Mwandishi Wetu-Zanzibar



UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umechambua utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya saba ya Dk. Ali Mohamed Shein na kuitaja ni yenye mafanikio sambamba na ukuzaji wa uchumi na demokrasia visiwani Zanzibar.

Kutokana na hali hiyo vijana wa UVCCM wametakiwa kuipa kila aina ya ushirikiano Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hasa katika kuhakikisha inawaletea maendeleo wananchi wote.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Zanzibar na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa viongozi vijana wa ngazi za matawi hadi mkoa yaliyofanyika katika Ofisi ya CCM Mkoa Amani Mkoa wa mjini Magharibi kisiwani unguja.

Alisema sifa kubwa ya CCM ni kutoa viongozi wenye weledi, upeo na uwezo thabiti wa kuwaongoza wananchi na kuwatumikia kwa haki bila kuongozwa na msukumo wa ukabila, nasaba au asili za watu.

Alisema nje ya CCM utakutana na viongozi ambao wana utamaduni wa kuhubiri siasa za mgawanyiko katika jamii, wanaopenda malumbano ambao hawana mikakati wala mbinu na maarifa ya ubunifu wa mambo mazuri yenye tija na manufaa kwa wananchi.

“Rais Dk. John Magufli na Dk. Shein ni vielelezo katika kudumisha uongozi wa haki uliotukuka, unaojali maslahi ya umma, wenye kutambua dhana ya uwajibikaji na kuwatumikia wananchi kwa misingi ya uwazi na haki,” alisema.
Alisema mambo yaliyofanyika zanzibar kimaendeleo katika awamu ya saba hayahitaji ushahidi bali yanahitaji kuungwa mkono na wale wanaojaribu kuyabeza na kujifanya hawaoni lazima waonywe hadharani bila kuwaonea muhali na kuelimishwa.

“Serikali ya CCM inasifa ya kutenda na kuwajibika kuliko kusema kwasababu wameaminiwa na wananchi. Jukumu la kusema wapo wanasiasa wenye uhodari wa kuropoka maneno lakini wamepungukiwa na uwezo wa kutenda na kutekeleza lolote,” alisema.

Kaimu Katibu Mkuu alisema vijana wa CCM ndiyo wanatakiwa kuwa wa kwanza kunadi utelekezaji wa ilani ya uchaguzi na kuzungumzia mema yote yanayofanywa na Serikali zao kwani hilo jukumu lao la awali.
“Kila kiongozi anawajibu wa kukitumikia chama chetu wakati wote bila kusukumwa.

Awe mwenye ujasiri wa kupiga vita rushwa na ufisadi , awe mzalendo kwa nchi yake na anayejituma bila kuhitaji malipo au ujira,” alististiza Shaka
Awali Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini, Kamaria Nassor, alisema wamejipanga vyema kutekeleza maazimio na maelekezo yanayotolewa na jumuiya ili kuibua uhai na vuguvugu kwa vijana sambamba na kujiandaa vyema na uchaguzi wa 2020 ambao wanaimani CCM itashinda kwa kishindo kikubwa.

“Sisi ni vijana tunaojielewa na kujitambua tumeamua kutekeleza maagizo na maelekezo yenu viongozi wetu hasa kauli mbiu ya tukutane kazini ya mwenyekiti Kheir Jemes tumejipanga vyema kuitekeleza kwa vitendo na tunaimani tutafanikiwa kutekeleza mipango yetu mbalimbali tuliyojiwekea mkoani kwetu vijana,” alisema Kamaria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles