24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM WAWAASA VIONGOZI ‘WADOKOZI’

Na Mwandishi Wetu-NGARA


shaka-hamdu-shakaUMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), umesema miradi, mali na vitega uchumi vyake ni miliki ya chama hicho.

Kutokana na hali hiyo, umoja huo umewaasa viongozi wanaouza mali za chama, wadokozi na wanaojimilikisha kinyume cha sheria, kutambua siku zao zinahesabika.

Pia umoja huo umewataka viongozi wa jumuiya kuanzia sasa kuheshimu, kutunza na kukaa mbali na mali hizo, yakiwamo majengo, mashamba, viwanja na vitega uchumi mbalimbali.

Msimamo huo, ulitolewa jana katika Kijiji cha Bugarama, Wilaya ya Ngara mkoani hapa na Kaimu Katibu Mkuu wa UCVVM, Shaka Hamdu Shaka, wakati akizindua shamba la umoja huo na kupanda miti 70.

Shaka, aliwaasa vijana wa umoja huo popote walipo kufuta ndoto za kutaka kutajirika kwa njia za mkato, bila kutoka jasho.

“Huu ni mtazamo hasi usiofaa kufuatwa na wala kuigwa, shamba hili si la viongozi wa UVCCM, bali ni miliki ya chama, msicheze na chama, atakayekiibia ataaibika, atafikishwa mahakamani na pengine si ajabu akafungwa jela,” alisema .

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ngara, Faris Mohamed, alisema chini ya uongozi wake hakuna mtu  mwenye jeuri ya kupora mali ya jumuiya hiyo.

Alisema umoja huo wilayani Ngara utafanya kila linalowezekana kuhakikisha jumuiya yao inajijenga kiuchumi na kuzitumia rasilimali mbalimbali zilizopo kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali na halmashauri ya wilaya .

“Nitaheshimu na kulinda mali zetu, sitaona haya kumshughulikia mtu yeyote ambaye atajifanya ana mikono mirefu ya kukwapua, sitautia madoa uongozi wangu kwa tamaa za kupita,” alisema Faris.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles