27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

WABUNGE WA UPINZANI WAKWAMISHA BUNGE KENYA

NAIROBI, KENYA


 

KENYATTA
KENYATTA

WABUNGE wa muungano wa upinzani wa Cord, jana walikwamisha shughuli za Bunge la Taifa kwa saa mbili, wakipinga kufanyika kwa kikao maalumu kilichoitishwa na Spika Justin Muturi.

Wabunge walimzuia Muturi kwenda kukaa eneo lake, wakisema kikao hicho kilichopangwa kuanza saa 3.30 asubuhi kilikuwa haramu kwa vile viongozi wao wa Bunge hawajashirikishwa.

Waliapa kuendelea kuziba njia hadi Muturi atakaposhauriana na viongozi wao wa Bunge, ambalo limetawaliwa na muungano unaotawala wa Jubilee.

Wakati wote huo wa mkwamo, kulikuwa na utitiri wa polisi katika majengo ya Bunge, huku maofisa wakizuia magari kupita barabara ya Bunge.

Aidha rungu la Bunge lilionekana kuwa chombo kilichokuwa kikilindwa zaidi na walinzi wa pande zote mbili bungeni.

Bunge lilikuwa lijadili sheria na kanuni ambazo zitasimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2017.

Jubilee na Cord wanavutana kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya sheria za uchaguzi na kanuni nyinginezo.

Wakati ushirika wa Jubilee ukitaka sheria zibadilishwe kuendana na ‘uhalisia’, Cord wanataka zibaki zilivyo na wanautuhumu ushirika wa Rais Uhuru Kenyatta kuwa na nia mbaya.

Sheria hizo zilikubaliwa na wajumbe wa Kamati ya Haki na Masuala ya Kisheria kama sehemu ya mageuzi ya sheria ya uchaguzi kabla ya kufanyika uchaguzi mwakani.

Katikati ya mjadala huo, ni mapendekezo yaliyowasilishwa na kamati hiyo ya Samuel Chepkong’a kurekebisha sheria ya uchaguzi.

Mapandekezo hayo pamoja na mambo mengine, yanataka yataje kuwa iwapo matumizi ya teknolojia kama vile kazi za kuhesabu na kujumuisha kura kielektroniki itashindwa kufanya kazi, mfumo wa kawaida wa kuhesabu kura utumike kutambua wapigakura na kusambaza matokeo.

Maeneo mengine yaliyogusiwa ni ongezeko la idadi ya wapigakura katika vituo vya kupiga kura kutoka 500 hadi 700, kuondoa sifa za kielimu kwa wagombea na kuhusu sheria ya gharama za uchaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles