26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM Ilala wakabidhiwa vitendea kazi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM Kata ya Kisutu wametoa msaada wa kompyuta mpakato na printa kwa ofisi ya UVCCM Wilaya ya Ilala ili kurahisisha utendaji kazi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kisutu, Komail Rizwan, amesema wameguswa kutoa msaada huo kama sehemu ya kutatua baadhi ya changamoto zinazokabili ofisi hiyo.

Kada wa CCM, Tousif Bhojani (wapili kushoto), akikabidhi printa kwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala, Juma Mizungu. Kulia ni Katibu wa UVCCM Ilala, Jesca Msengi.

Amesema msaada huo umetolewa kwa ushirikiano wa kada wa chama hicho, Tousif Bhojani ambaye ameahidi kuendelea kutatua changamoto zinazokabili ofisi hiyo.

“Hii ni ofisi yetu hivyo tutahakikisha tunaijenga pamoja kwa kutatua changamoto mbalimbali zilizopo,” amesema Rizwan.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala, Juma Mizungu, ameshukuru kwa msaada huo kwani utasaidia kurahisisha utendaji wa shughuli za kila siku.

“Nafurahi sana mazingira ya ofisi yangu yanaboreshwa, hili ni jambo kubwa sana, mmetuheshimisha, tumepambana lakini kwingineko tumeahidiwa tu naomba tuendelee kuwa na moyo wa kukitumikia chama,” amesema Mizungu.

Mizungu amewaomba wanachama wengine waige mfano huo ili kuendelea kukijenga chama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles