25.3 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

UNHCR: Tanzania imefanikiwa kulinda amani

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

AFISA Muhifadhi Wakimbizi Mwandamizi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), nchini Tanzania, Boniface Kinyanjui amesema, Serikali ya Tanzania imefanikiwa kulinda amani yake.

Kinyanjui alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye warsha ya siku tatu na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, mjini Morogoro iliyoanza leo Novemba 23, 2022.

Sehemu ya Wahariri.

‘‘Amani haitoki juu kushuka chini, inalindwa na serikali, Serikali ya Tanzania imefanikiwa katika hili.…, Tanzania ni nchi ya amani lakini imezingirwa (na nchi zenye wasiwasi wa amani),’’ amesema Kinyanjui.

Ofisa huyo amesema, Tanzania ni nchi iliyohifadhi wakimbizi kwa muda mrefu tangu uhuru na kwamba, ni miongini mwa nchi chache mabazo ziliruhusu baadhi ya wakimbizi kuwa raia wake.

‘‘Tanzania imepokea wakimbizi kutoka Ulaya, Marekani na hata Kenya hapo. Ni miongoni mwa nchi chache zilizowapa wakimbizi uraia wan chi yake,’’ amesema.

Hata hivyo amesema, UNHCR hupenda zaidi zaidi kuona walimbizi wakipewa hifadhi pamoja na ruhusa ya kuendelea na maisha yao ya uzalishaji mali na si kuwekwa pamoja kwenye makambi.

‘‘Wakimbizi na watu wanaoomba hifadhi sio watu wanaopendwa sana katika nchi nyingi. Sisi tungependa kuona wakimbizi wakipewa nafasi ya kujimudu kimaisha katika uzalishaji mali maana ni wanadamu kama wengine.

‘‘Katika wakimbizi kuna wataalamu wengi ambao wanaweza kusaidia jamii. Mfano; kuna mkimbizi alitoka Sudani Kusini na lipita Tanzania akaenda Afrika Kusini. Huko yeye ndiye aliyetengeneza mfumo wa kutoa maji kwenye mwili kupitia tundu za pua wakati ule wa UVIKO-19,’’ alisema.

Akizungumzia shirika hilo, Kinyanjui aliema UNHCR ilianzishwa mwaka 1950 na kwamba, mwaka 1951 ndio ilianza kuingia mikataba ya amani

‘‘Lengo kubwa la UNHCR ni kulinda haki ya mfungwa na mahitaji yake kokote atakapokuwa,’’ ameongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,718FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles