25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

UTURUKI YAISHTAKI MAREKANI WTO

ISTANBUL, UTURUKI                  |                   


SERIKALI ya Uturuki imeishtaki Marekani katika Shirika la Kimataifa la Biashara (WTO) kwa hatua yake ya kuongeza ushuru wa bidhaa za chuma cha pua na bati kutoka nchini hapa.

Agosti 10 mwaka huu, Rais wa Marekani, Donald Trump, alitangaza kuwa ataongeza mara mbili viwango vya kodi kwa asilimia 50 kwa bidhaa za chuma cha pua kutoka Uturuki na bati kwa asilimia 20.

Uamuzi huo wa Marekani umekuja kufuatia mvutano unaoendelea, unaomhusu mchungaji wa Marekani, Andrew Brunson, anayeshtakiwa nchini hapa kwa makosa kadhaa ikiwamo ugaidi.

Katika barua yake kwa WTO, Uturuki inadai Marekani ilivunja sheria za biashara wakati ilipotangaza Juni mwaka huu kutoza kodi kwa asilimia 25 bidhaa za chuma cha pua na bati asilimia 10 kwa nchi nyingi isipokuwa Argentina na Australia pekee.

Kwa mujibu wa Serikali ya hapa, hatua ya hivi karibuni ya Marekani dhidi ya Uturuki inazidiasha ukiukaji huo wa sheria za WTO.

Wiki iliyopita, Uturuki ilitangaza kujibu hatua hiyo ya Marekani kwa kupandisha kodi kwa bidhaa 22 tofauti za taifa hilo, ikiwa ni pamoja na magari, mchele, vipodozi na tumbaku.

Chini ya sheria za WTO, Uturuki na Marekani sasa zina siku 60 kumaliza mvutano huo kwa njia ya mazungumzo na kama zitashindwa kufikia mwafaka, shirika hilo litalazimika kutoa uamuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles