|Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Uongozi wa Kampuni ya Bakhressa (BFPL), umeiomba Serikali kupunguza wingi wa taasisi za udhibiti ubora na kodi kubwa inayotozwa wakati wa uingizaji wa makasha maalumu ya kuhifandhia matunda.
Wito huo umetolewa leo na Meneja Uhusiano wa Bakhressa, Hussein Sufian wakati Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ilipotembelea kiwanda cha kusindika matunda na kutengeneza juisi kilichopo Mlandege wilayani Mkuranga.
Amesema utitiri wa tasisi hizo umekuwa kikwazo katika ukuajia wa viwanda nchini na kupunguza hamasa kwa wawekezaji wapya.
“Pia changamoto yingine inayotukabili ni hizi stika za kodi za kieletronic (ETS) na vikwazo visivyokuwa vya kikodi kwa bidhaa za Azam Mango na Azam energy kuuzwa kwa wateja nchini Kenya, haya ni baadhi ya mambo tunayoomba serikali iyashughulikie kwa umakini,” amesema.