26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Uswisi kuwalipa fidia waliokuwa watumwa

verdingkinder_2GENEVA, USWISI

WANASIASA nchini Uswisi wamepitisha sheria ya kuwalipa fidia waliokuwa watoto waliotumikishwa kazi ngumu wajulikanao kama Verdingkinder.

Chini ya sheria ambazo zilikuwapo hadi miaka ya 1980, maafisa waliwachukua watoto kutoka familia masikini, yatima, watoto waliozaliwa nje ya ndoa, ambao wazazi wao walikuwa walevi au walitengana na kuwalazimisha kufanya kazi ngumu za sulubu.

Katika jitihada za kujaribu kukabili moja ya doa kubwa katika historia ya Uswisi, juzi Bunge liliidhinisha fidia kwa maelfu ya watu ambao walitenganishwa na familia zao wakiwa watoto.

Serikali ina mipango ya kutumia Faranga milioni 308 za Uswisi kuwalipa fidia kati ya waathirika 12,000 hadi 15,000 ambao bado wako hai.

Kila mmoja atapokea kati ya Faranga 20,000 hadi 25,000. Faranga moja ya Uswisi ni sawa na Sh 2,270 za Tanzania

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles