Na WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM
BAADHI ya watu wamekuwa wakiandaa chakula kwa kuweka chumvi nyingi, jambo ambalo si zuri kiafya.
Ni ukweli usiopingika kuwa chumvi ni kiungo kikuu katika chakula, kwani licha ya kukipa radha, pia kiungo hiki hutupatia madini (sodium) mwilini, lakini kinapotumika vibaya kinaweza kuleta madhara makubwa.
Hakikisha unaweka chumvi kiasi kwenye chakula ili kujiepusha na tatizo la shinikizo la damu na magonjwa mbalimbali ya moyo.
Kitaalamu tunashauriwa kutumia chumvi yenye madini joto ili kudhibiti kiwango cha sukari mwilini na kujiepusha na magonjwa mbalimbali kama vile Goita unaosababishwa na matumizi ya chumvi isiyokuwa na madini joto.